PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

AyoTV

Hakuna mabadiliko, JKT Tanzania vs Yanga watacheza Mkwakwani tu!!

on

Baada ya maneno maneno kuwa mengi na baadhi ya watu kuhoji kwa nini mchezo wa JKT Tanzania dhidi ya Yanga huchezwe uwanja wa Taifa Dar es Salaam na sio uwanja Mkwakwani kama ilivyokuwa katika game ya JKT Tanzania dhidi ya Simba SC.

Shirikisho la soka Tanzania limetoa tamko kuhusiana na baadhi ya watu wanaohoji kwa nini mchezo wa JKT Tanzania dhidi Yanga huchezwe uwanja wa Taifa wakati JKT waliomba uwanja wao wa nyumbani kwa mechi za Simba na Yanga uwe CCM Mkwakwani Tanga.

Afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo ametolea ufafanuzi taarifa hizo na kueleza kuwa mchezo utakaochezwa Dar es Salaam kati ya JKT Tanzania na Yanga ni mchezo ambao JKT Tanzania atakuwa mgeni lakini mchezo wao wa marudiano February 9 2019 utachezwa uwanja wa Mkwakwani kama ilivyopangwa hakuna mabadiliko yoyote.

EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?

Soma na hizi

Tupia Comments