Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U HEARD: Muigizaji wa Bongo Movie aliyenasa ujauzito baada ya kusema amebakwa

on

Leo November 21, 2016 U Heard ya XXL ndani ya Clouds FM imempata muigizaji wa Bongo Movie anayefahamika kwa jina la Nisha ambaye ana stori kuhusu ujauzito alioupata kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake na inaelezwa ni msanii wa BongoFlava. 

Stori haikushia kwenye ujauzito pekee, kwa mujibu wake Nisha amedai kwamba alibakwa na mwanaume huyo akiwa hajitambui baada ya kuachana na alipotaka warudiane yeye Nisha alikataa jambo hilo na ndipo mwanaume huyo akatumia njia za kumrubuni na kumbaka.

Nisha amefunguka kwa kueleza kuwa kwasasa hata hataki mwanaume huyo ajue kwamba yeye ndiye mwenye ujauzito huo.

“Sijabakwa kama ambavyo wengi wamekuwa wakisema hivyo, ila pia nimebakwa kutokana na mazingira yaliyojitokeza, alikuwa boyfriend wangu tukaachana yeye akataka turudiane nilikataa akatumia njia anazozijua yeye kunirubuni likatokea la kutokea nimekuja kushtukia tayari ni mjamzito” – Nisha

Unaweza kuiskiliza full stori hapa. Bonyeza play

VIDEO: Yapo hapa majibu ya Shamsa Ford kuhusu walivyokuwa wapenzi na Nay wa Mitego. Bonyeza Play kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement