Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Mambo matano aliyozungumza Papii Kocha, ‘Niliacha mpenzi nimekuta anamtu”

on

Msanii Papii Kocha amehojiwa leo kupitia kipindi cha Leo tena ya Clouds FM akiwa pamoja na Baba yake Babu Seya ambapo amezungumza baadhi ya mambo kuhusu wao, wakati wakiwa Gerezani na mpaka walipotoka ikiwa ni miaka 14 tangu wawe uraiani.

Papii amesema kwamba wakati alipokuwa Gerezani alikuwa kwenye kitengo cha washonaji kofia na alijifunza kule kwa sasa anajua vizuri, lakini pia amesema kwamba aliacha mwanamke na mtoto wa miaka 4 lakini saivi katoka kamkuta ana miaka 18 na mwanamke wake aliyemuacha kakuta yupo na mtu mwingine.

“Niliacha mtoto anaitwa Aisha tulikuwa tunaishi pamoja na mama yake wakati naenda jela nilimuacha ana miaka minne, nimemkuta ana miaka 18 wakati nilipokuwa kule alikuwa anakuja japo siyo sana kwani muda mwingi alikuwa shule, mama yake alikuwa anakuja kuniona nilivyotoka mama yake naonana nae ni mzazi mwenzangu nimerudi nimemkuta na mtu wake miaka 14 siyo mchezo.”

“Hiyo hali nimeipokea kawaida maana kifungo chenyewe kilikuwa kinatisha sasa mwingine anaona labda nilikuwa nisitoke so maisha mengine lazima yaendelee hajafanya makosa kwa maamuzi yake maana maisha mengine lazima yaendelee.”

“Nakumbuka show yangu ya mwisho kubwa niliyowahi kuifanya ilikuwa ni Fiesta nyingine watu watakutana nayo kesho pale kingsolomoni.”

“Mimi na mzee wangu tunabahati sana siyo mchezo toka tupo gerezani mpaka sasa, ndugu zangu wananisaidia kwenye kujifunza kutumia mitandao ya kijamii kama Instagram ila whatsapp natumia mwenyewe mitandao mizuri lakini kama ukitumia vibaya inakuwa shida kidogo.”

“Jambo linalonishangaza toka nimetoka ni mwendo kasi sijapanda ila natamani sana kupanda mwendo kasi sijazunguka kabisa lakini ntaenda daraja la kigamboni kupiga picha, kule gerezani umeme ukikatika  hazipiti dakika mbili lazima urudi kuna jenereta”

LULU DIVA “Kapokonywa vitu, Saizi ametelekeza mtoto !!!”

EBITOKE: Kuhusu Mama Ashura kutoonekana, ‘chizi kiziwi’ kam-block

Soma na hizi

Tupia Comments