Michezo

Mtoto wa Cristiano Ronaldo kwenye rekodi “Like Father Like Son”

on

Like Father Like Son mtoto wa Cristiano Ronaldo anayejulikana kwa jina la Cristiano Ronaldo JR anayeichezea club ya vijana ya Juventus, tayari ameanza kuingia kwenye headlines kama baba yake kutokana na uwezo wake anaoendelea kuuonesha akiichezea Juventus.

Cristiano Ronaldo JR mwenye umri wa miaka 8 kwa sasa anaendelea kufanya vizuri katika soka, sasa akiwa na timu ya watoto ya Juventus hadi sasa amecheza game 23 na kufanikiwa kufunga magoli 58 na kutoa assist 17 katika michezo hiyo.

Kutokana na kiwango hicho alichokionesha na kufanya kuwa gumzo mitandaoni, sasa uwezo wake na mechi alizocheza ni swa na wastani wa kufunga magoli zaidi ya mawili katika kila game, hata hivyo mtoto huyo amekuwa na utamaduni wa kufunga mipira ya faulo kama ilivyo kwa baba yake na hata ushangiliaji wake.

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments