Tangaza Hapa Ad

Michezo

FA imempa siku 3 Jose Mourinho ajitetee kwa tuhuma za utovu wa nidhamu

on

Mchana wa leo November 28 2016 chama cha soka nchini England FA walitangaza kuliona tukio la Jose Mourinho kupiga chupa ya maji kwa hasira wakati wa mchezo kati ya Man United dhidi ya West Ham United uliomalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.

FA walisema wanasubiri kwanza ripoti ya refa wa mchezo ule Jon Moss ambaye alimuamuru Jose Mourinho kutoka katika benchi kufuatia tukio la kupiga chupa kwa hasira dakika ya 27 ya mchezo, baada ya kuona Paul Pogba anaoneshwa kadi ya njano kwa kudaiwa kujiangusha.

Kama utakuwa unakumbuka Jose Mourinho hilo litakuwa kosa la pili kulifanya ndani ya mwezi mmoja, baada ya October 29 kutolewa katika benchi katika mchezo dhidi ya Burnley na baadae  FA ikampiga faini ya pound 8,000 na kufungiwa mechi moja kukaa katika benchi.

Jose Mourinho pia alipigwa faini ya pound 50,000 wakati wa mchezo dhidi ya Liverpool October 17 2016 baada ya kuadhibiwa kosa la kumtolea maneno machafu refa Anthony Taylor.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement