Tangaza Hapa Ad

Michezo

Hii haiwezi kuwa habari njema kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu Cazorla

on

Kama ni shabiki wa timu ya Arsenal ya England najua huwezi kufurahishwa na habari zilizoripotiwa leo December 1 2016 kuhusiana na kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea timu hiyo Santi Cazorla.

Taarifa kutoka BBC zinaeleza kuwa Cazorla atafanyiwa upasujai wa kifundo cha mguu (enka), upasuaji ambao utamfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu, kiungo huyo hajaichezea Arsenal toka katikati ya mwezo October baada ya ushindi wa Arsenal wa goli 6-0 dhidi ya Ludogorets mchezo wa UEFA.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Cazorla msimu uliyopita alikosa kuichezea Arsenal kwa miezi saba, kutokana na kuwa na jeraha la goti, Cazorla ambaye ameichezea Arsenal mechi 11 na kuifungia magoli mawili katika mashindano yote msimu huu, atafanyiwa upasuaji Sweden wiki ijayo.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement