Biko


Tangaza Hapa Ad

Top Stories

“Kama Serikali haitafanya chochote, tutaandamana mpaka ubalozi wa Marekani”- ACT Wazalendo

on

Chama cha ACT Wazalendo kimetaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya rais  wa Marekani Donald Trump kufuatia hatua yake ya kutoa matamshi ya chuki dhidi ya mataifa ya Afrika na raia wanaotoka bara la Afrika.

Akiongea na AyoTV na millardayo.com Mkurugenzi wa kamati ya masuala ya kigeni katika chama hicho Vennace Msebo ametaka Waafrika kuungana kwa pamoja kupinga matamshi hayo.

“Hatukubaliani na matamko ya namna hii, tumeiandikia barua Serikali kupitia Wizara ya Mambo Nje kuiomba iwaambie Umoja wa Afrika kuwa Rais Trump anatakiwa kuwaomba msamaha Waafrika, kama Serikali haitafanya chochote tutaandamana mpaka ubalozi wa Marekani,”– Venance Msebo

MKUU WA WILAYA ALIVYOWAONGOZA WANANCHI KUJENGA MADARASA KWA AJILI YA WATOTO 422

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement