Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

MAHAKAMANI: Jalada la walioisababishia Serikali hasara ya Bilioni 2 lafika kwa DPP

on

Leo February 13, 2018 Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi ya uhujumu uchumi wa kuisababishia hasara serikali ya Bilioni 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini, Archard Kalugendo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya uchunguzi.

Mbali ya Kalugendo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu.

Wakili wa serikali,  Estezia Willson amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamikika.

Pia ameeleza kuwa jalada halisi la Kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya uchunguzi. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi February 27,2018.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababisha serikali hasara ya zaidi ya Bilioni 2.4.

Inadaiwa kuwa kati ya August 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.

ALICHOZUNGUMZA DIAMOND PLATNUMZ NA HAMISA BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

 

Soma na hizi

Tupia Comments