Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Agness ‘Masogange’ Mahakamani tena leo na unachotakiwa kufahamu (+picha 5)

on

Mrembo Mtanzania Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amekua na kesi Mahakamani ambayo imekua ikiendelea siku hadi siku ambapo leo alirudi tena Mahakamani na kilichoendelea ninacho.

Taarifa ikufikie tu kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea vielelezo vya sampuli ya mkojo wa Agnes Gerald ‘Masogange‘ kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali August 28 2017.

Kesi hiyo imetolewa ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ambapo upande wa mashtaka uliomba kielelezo cha ushahidi wa mkojo wa Masogange kipokelewe.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko alidai wanapinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kwa sababu Polisi walitakiwa kuiomba Mahakama ili wachukue vipimo vya Mshitakiwa lakini hawakufanya hivyo ambapo ni kinyume na sheria 63 CPA.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri aliahirsha kesi hiyo hadi August 28/2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi ambapo hizi hapa chini ni picha za leo Agness Masogange akiwa kwenye eneo la Mahakama.

KWANINI WEMA SEPETU HAJAKABIDHIWA KADI YA CHADEMA JANA? Play hapa chini kufahamu kila kitu

WEMA SEPETU MAHAKAMANI KUHUSU KESI YAKE… PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments