Tangaza Hapa Ad

Stori Muhimu

Miezi tisa hakuna majibu ya ndege ya Malaysia Airlines 370, nyingine imepotea leo…

on

aa_mBado Dunia imebaki njia panda juu ya wapi ilipo ndege ya Malaysia Airlines 370 ambayo ilikuwa na abiria 239, ilipotea miezi zaidi ya nane iliyopita ikitokea Malaysia kwenda China, ndege nyingine imepotea, ilitokea Singapore kwenda Indonesia.

Iliyopotea saa chache zilizopita ni AirAsia qz 8501, ilikuwa na abiria 162 wengi wao walikuwa raia wa Indonesia na Uingereza imethibitisha kuwa kuna mtu mmoja raia wa nchi hiyo alikuwa akisafiri na mtoto wake.

Ndege ilipotea wakati rubani alipolazimika kubadili mwelekeo wa ndege hiyo pasipo kuomba mwelekeo kutoka kwa waongozaji kutokana na hali mbaya ya hewa.

Ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo wamejikusanya katika uwanja wa ndege wa Surabaya Indonesia, wakisubiri kupata taarifa yoyote itakayokuwa na matumaini kwao.

Baadhi ya vikosi vinavyotafuta ndege hiyo vimesitisha zoezi hilo kutokana na hali mbaya ya hewa huku vingine vikiendelea.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments

Advertisement