Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Alichoandika mwimbaji Christina Shusho kwa Paul Makonda

on

Christina Shusho ni moja kati ya waimbaji maarufu wa muziki wa injili Tanzania ambao wamefanikiwa kufikisha pia kazi zao nje ya Tanzania. Christina amekuwa na utaratibu wa kuandika jumbe kwa baadhi ya viongozi na watumishi mbalimbali wa dini. Leo Jan 16 ametumia ukurasa wake wa Instagram na kumuandikia mkuu wa mkoa wa Dar es laam, Paul Mkonda

>>>I thank God for your life in christ, mhe @paulmakonda, wengi wana kujua kwa mengi na sifa nyingi ulizo nazo. Katika maombi yetu leo tuna simama na wewe kama mwana wa Mungu, balozi wa siri za kristo, tuna kuombea mwaka huu ukawe mwaka wako utakapo imba wimbo mpya.
>>>Mwaka huu@paulmakonda Mungu akupe haja ya moyo wako, mwaka huu @paulmakonda ukumbukwe na Mungu, mwaka huu Mungu akupe kicheko, mwaka huu Mungu abadili jina lako na kukupa jina jipya….KUMBUKA UTAKAPO KULA, KUNYWA na KUSHIBA usi msahau Bwana Mungu wako.
>>>Mungu aongoze hatua na miguu yako, hekima ya Mungu iwe juu yako, uka ongoze wana dar es salaam kwa upendo, upate kibali mbele ya Wakuu na watu unao waongoza..
Mtangulize Mungu kwa kila jambo..
jina la Yesu litukuzwe AMEN – Christina Shusho

Video : Kama ulipitwa na uchambuzi wa magazeti ya leo Jan 16 yakisomwa na David King AyoTV>>>

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement