Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

BREAKING: Rais Magufuli amemteua Mnadhimu Mkuu Wa JWTZ

on

Taarifa niliyoipokea kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ikulu ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo February 14, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pamoja na uteuzi huo, Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Aidha, Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali kama ifuatavyo

  1. Brig Jen. J.G. Kingu
  2. Brig Jen. M.S. Busungu
  3. Brig Jen. R.R. Mrangira
  4. Brig Jen. B.K. Masanja
  5. Brig Jen. G.T. Msongole
  6. Brig Jen. A.F. Kapinga
  7. Brig Jen. K.P. Njelekela
  8. Brig Jen. A.S. Bahati
  9. Brig Jen. M.E. Mkingule
  10. Brig Jen. S.S. Makona

Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye. Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho February 15, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Alichojibu Kamanda Kinondoni kuhusu Madai ya CHADEMA kuvamiwa na Polisi

 

Soma na hizi

Tupia Comments