Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: DR Congo walivyolazimishwa sare ya 2-2 na Ivory Coast AFCON 2017

on

January 20 2017 michezo ya Kundi C ya michuano ya mataifa ya Afrika 2017 maarufu kama AFCON 2017, imeendelea Oyem nchini Gabon, ambapo michezo ya Kundi C inachezwa.

Leo mchezo wa kwanza ulikuwa ni Ivory Coast dhidi ya DR Congo ambayo kama ingepata ushindi leo ingefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya AFCON 2017 moja kwa moja, kwani ingekuwa inafikisha point sita.

Mchezo wa Ivory Coast dhidi ya DR Congo ni mchezo ambao umemalizika kwa timu kutoshana nguvu, kwani DR Congo imelazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Ivory Coast.

Congo ndio walianza kufunga goli la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa Neeskens Kebano, lakini Wilfred Bony aliisawazishia Ivory Coast dakika mbili baadae, Junior Kabananga akaifungia Congo goli la pili ambalo Ivory Coast, walifanikiwa kusawazisha dakika ya 67 kupitia kwa Geoffroy Serey Die.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement