Tangaza Hapa Ad

Michezo

CONFIRMED: Mchezaji wa KRC Genk aliyechukuliwa na Bayer Leverkusen

on

Ni kutoka Ubelgiji ambako Tanzania pia inae Mtanzania Mbwana Samatta anaeichezea timu ya soka ya KRC Genk ya Ubelgiji ambapo habari kubwa kwa sasa kuhusu club hiyo ni kuhusu Mjamaica Leon Bailey.

Rasmi leo January 31 2017 Mjamaica huyo amejiunga na Bayer Leverkusen ya Ujerumani aliyekuwa anaunda safu ya ushambuliaji ya Genk na mtanzania Mbwana Samatta ametambulishwa rasmi na Bayern.

Leon Bailey mwenye umri wa miaka 19 anaondoka KRC Genk na kujiunga na Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa mkataba wa miaka mitano hivyo atakaa katika klabu hiyo hadi 2022 ambapo anaondoka KRC Genk akiwa kaitumikia kwa mwaka mmoja na nusu.

Kama utakumbuka, Leon Bailey alikuwa akiwaniwa na Time kadhaa ikiwemo Man United, Hull City lakini Bayer Leverkusen ndio wamefanikiwa kumsajili kwa dau la pound milioni 11 na anakuwa staa wa pili wa KRC Genk kuondoka January hii baada ya Wilfred Ndidi aliyejiunga na Leicester City.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement