Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Ndani ya mkutano Lucky Vicent Arusha kabla ya Polisi kuvamia (+video fupi)

on

Leo May 18 kwenye shule ya Lucky Vicent Arusha, Polisi walivamia mkutano ulioongozwa na Meya wa jiji hilo akiambatana na viongozi wa dini, Madiwani na Waandishi wa habari ambao Meya alidai lengo lake ni kukabidhi rambirambi walizozichanga wao kutokana na msiba wa ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Wakati viongozi hao wakiendelea kuhojiwa na Polisi Arusha, millardayo.com na AyoTV zinakukutanisha na video ya sehemu ya vilivyokua vinazungumzwa ndani ya mkutano huo kabla ya Polisi kuvamia.

Hii video hapa chini Katibu wa chama cha Wamiliki wa Shule binafsi mkoa wa Arusha Leonard Mao alikua anaongea >>> “Nilitangaza kwa niaba ya Watanzania siku ya kuaga ile miili 35 kwamba tutaendelea kuchanga rambirambi zetu na kwenda kuwaona wale wazazi mmoja baada ya mwingine

“Hakuna hata senti ya mtu itakwenda pembeni…. hatumpi mtu hata kwenye shule ya Vicent, ni waliofiwa wenyewe mkono kwa mkono’ FULL VIDEO NDIO HII HAPA CHINI UNAWEZA KUPLAY UKAJIONEZA ZAIDI

Kumekuwepo na gumzo kuhusu ishu ya Rambirambi za msiba wa ajali ya Wanafunzi Arusha ambapo juzi Meya wa Arusha alimpa siku 3 Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo kutoa taarifa kamili kuhusu rambirambi zilizotolewa.

VIDEO: Vilio na huzuni, miili 32 ikiagwa Arusha…. tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Lowassa afunguka, kongamano kukataliwa, Rais Magufuli, vyeti feki na mengine…. play hapa chini kutazama

USIKUBALI !! usikubali kupitwa na chochote… Ripota wako wa nguvu Millard Ayo yuko tayari kukukutanisha na matukio yote ya BREAKING NEWS, MICHEZO, HABARI ZA MASTAA na mengine, cha kufanya ni kumfollow kwenye Instagram, Facebook, Twitter, subscribe Youtube na ku-install APP ya ‘millardayo‘ kwenye Android na IOS.. kote huko utampata kwa jina hilohilo moja la ‘millardayo’

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement