Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba imelazimishwa sare na Mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup

on

Wekundu wa Msimbazi Simba leo wameshuka uwanjani kucheza dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wake wa tatu wa Kundi A wa Kombe la Mapinduzi, Simba waliingia kucheza dhidi ya URA wakiwa wameshinda michezo yao miwili ya mwanzo.

Wakati Simba wakiingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mchezo wao wa mwisho, URA wao waliingia wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa goli 2-1 dhidi ya Jang’ombe Boys kabla ya kukutana na Simba leo katika mchezo uliyomalizika kwa sare ya kutofungana.

Kwa sasa Simba anafikisha jumla ya point 7 na kuongoza msimamo wa Kundi A wenye timu za Jang’ombe Boys aliye nafasi ya pili kwa point 6, URA nafasi ya tatu kwa kuwa na point nne, Taifa Jang’ombe nafasi ya nne kwa kuwa na point tatu wakati KVZ wakishika mkia kwa kukosa point hata moja.

Simba sasa atarudi uwanjani Janury 8 kucheza dhidi ya Jang’ombe Boys katika mchezo wake wa mwisho wa Mapinduzi Cup 2017, wakati URA wao watarudi uwanjani siku hiyo hiyo kucheza dhidi ya Taifa Jang’ombe saa 20:15 usiku.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement