Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Yusuf Manji kwa mara nyingine ameshindwa kufika Mahakamani

on

Mfanyabiashara Yusuf Manji leo August 18, 2017 ameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya uhujumu uchumi kwa sababu za kiafya.

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati shauri lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo alidai kuwa amepata taarifa kutoka kwa Askari Magereza kwamba Manji anaumwa na amepewa (AD) ya siku mbili.

Licha ya Yusuf Manji kutofika Mahakamani kwa sababu za kiafya, washtakiwa wenzake Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere walifika ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi August 25, 2017.

Tazama kwenye video hii kuna kila kitu!!!!

ULIPITWA? Mashtaka 7 aliyosomewa Yusuf Manji akiwa Hospitali…tazama kwenye video hii!

ULIPITWA na kisa cha Yusuf Manji kumkataa Wakili Kibatala kusimamia kesi yake? Play kwenye video hii kutazama zaidi…

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement