Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Aubameyang alivyoinusuru Gabon na kipigo dhidi ya Burkinafaso

on

Jumatano ya January 18 2016 mwenyeji wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 maarufu kama AFCON timu ya taifa ya Gabon, ilicheza mchezo wake wa pili wa Kundi A katika uwanja wa Stade de Amitie dhidi ya Burkinafaso.

Gabon ambaye yupo nyumbani na anategemewa kufanya vizuri kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa mashabiki kuliko taifa lolote lile, amejikuta akiambulia sare ya pili mfululizo, baada ya kufungana na Burkinafaso goli 1-1.

Huu ni mchezo ambao Gabon walianza kufungwa dakika ya 22 kupita kwa Niguimbe Nakoulma ila jitihada za mshambuliaji wao mahiri Pierre Emerick-Aubameyang ziliisaidi timu hiyo kupata penati dakika ya 37 na kuisawazishia timu hiyo, matokeo hayo yanalifanya Kundi A hadi sasa kutokuwa na timu iliyopata ushindi toka michuano ya mwaka huu ianze.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement