Tangaza Hapa Ad

Michezo

MO Dewji muda mchache baada ya wanachama 1216 wa Simba kuridhia mabadiliko

on

Mfanyabiashara na bilionea w 16 Afrika Mohammed Dewji ni mmoja kati ya wanachama wa Simba SC ambao wanaunga mkono mabadiliko ya uendeshaji wa club ya Simba SC kutoka mfumo wa sasa na kuingia mfumo wa hisa.

Leo August 20 2017 muda mchache baada ya taarifa kutoka kuwa mkutano mkuu wa Simba SC umeridhia Simba na kuingia katika mfumo wa hisa kwa wajumbe 1216 waliyohudhuria mkutano huo kuunga mkono na mmoja pekee kusema hapana, MO Dewji ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe ambao unaashiria ni mtu mwenye furaha.

“Washabiki wa Simba hamjambo? Jumapili inaendaje? ?”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mohammed Dewji ndio mwanachama wa Simba aliyetoa wazo kuwa Simba iendeshwe katika mfumo wa kisasa wa hisa na kama Simba ikikubali, MO aliahidi kuwa ataomba auziwe asilimia 51 ya hisa za Simba kwa bilioni 20.

VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement