Tangaza Hapa Ad

Michezo

Azam FC imemtambulisha Abdul Mohamed aliyekuwa BBC

on

Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati klabu ya Azam FC leo October 6 2016 imetangaza rasmi kuongeza nguvu katika safu ya uongozi wa klabu hiyo, Azam FC ambao wanashiriki Ligi Kuu Tanzania bara na wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi hiyo wamemtambulisha meneja mkuu wa klabu hiyo

Kupitia kwa afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ametangaza Azam FC kuingia mkataba na mtangazaji wa zamani wa Clouds na BBC Abdul Mohamed kama General Manager wa klabu hiyo, lengo wa likiwa ni kusaidiana majukumu sambamba lakini kwa kuzingatia weledi.

“Abdul Mohamed ni mwenzetu tunamtambulsha rasmi kabisa kuwa ni mwenzetu ameingia katika familia ya Azam FC takribani mwezi mmoja uliopita, tupo nae anaingia katika sekretarieti ya Azam FC kama general manager” >>> Saad Kawemba

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement