Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Kilichofanya RC Kagera kumuweka ndani Afisa kwa saa 48

on

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu ameagiza kuwekwa ndani Afisa Mazingira Wilaya ya Biharamulo Michael MKuti kwa siku mbili kutokana na uzembe anaouonyesha katika kutekeleza majukumu ya Idara yake.

Maagizo hayo ameyatoa akiwa wilayani Biharamulo kwenye ziara ya kikazi kukagua miradi ya maji ambapo amesema kuwa afisa huyo amekuwa akionyesha uzembe katika Idara yake hali iliyopelekea miradi mingi kukwama na kusababisha wananchi kukosa huduma zao kimsingi.

Aidha, ameongeza kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira katika Wilaya ya Biharamulo na Mkuti ameshindwa kuwachukulia hatua wanaosababisha uharibifu huku akishindwa kuonekana kazini kwa kusingizia kuwa anaumwa. Full video nimekuwekea hapa chini tayari…

MAGAZETI: Maajabu Moto ulioteketeza soko, Usiyoyajua sakata la shamba la Sumaye 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement