Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Vipengele 16 vya MO Simba Awards 2018

on

Mwekezaji katika clab ya Simba, Mohammed Dewji  leo ametangaza rasmi kuwa ameamua kuanzisha tuzo za MO Simba Awards ambazo zitakuwa zikitolewa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa clab ya Simba.

Kwa mara ya kwanza tuzo hizo zitatolewa siku ya Jumatatu June 112018 katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam, tuzo zitakuwa na vipengele 16, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka.

MO Dewji

Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka na Tuzo ya Heshima, Tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Tuzo ya Benchi la Ufundi.

Kiongozi Bora wa Mwaka, Tuzo ya Wasimamizi wa Mchakato wa Mabadiliko, Mhamasishaji Bora wa Mwaka katika Mitandao ya Kijamii, Mhamasishaji Bora wa Mwaka na Tawi Bora la Mwaka, washindi watapatikana kwa kura zitakazopigwa mosimbaawards.co.tz na kamati ya tuzo.

“Simba ni timu kubwa inastahili kuwa na tuzo zake ambazo zitakuwa zinatolewa kwa kutambua mchango wa wenzetu ambao umetuwezesha kupata mafanikio haya ikiwepo kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ni jambo ambalo litawatia moyo kuendelea kujituma lakini hata kwa ambao watakosa itawatia hamasa na hivyo kuongeza juhudi”>>> MO Dewji

AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA

Soma na hizi

Tupia Comments