PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Hazard kazi kwake Chelsea wamemuwekea mkataba mezani

on

Club ya Chelsea leo usiku wa December 5 2018 itacheza game yake ya Ligi Kuu England dhidi ya Wolves wakati ambao mtaani zinazidi kutanda tetesi kuhusiana na staa wao raia wa Ubelgiji kama ataondoka Chelsea January au ataendelea kuitumikia club hiyo.

Chelsea inaonesha dhamira ya dhati ya kumuhitaji Eden Hazard aendelee kuitumikia timu yao lakini inaonekana kama ana nia ya kuondoka katika kikosi hicho na kwenda Hispania katika club ya Real Madrid kama ambavyo amekuwa akihusishwa nayo kwa muda mrefu sasa.

Kuelekea mchezo dhidi ya Wolves kocha Mkuu wa Chelsea Maurizio Sarri ameeleza kuhusiana na ishu ya Hazard ambayo imekuwa ikulizwa kwa muda mrefu sasa ila kwa upande wake amekiri kuwa anahitaji bado huduma ya staa huyo “Kiukweli mimi bado namuhitaji lakini namtaka abaki katika timu hii kama mwenyewe atapenda kubaki, majadiliano kati ya meneja wa Eden na Club yamekuwa yakifanyika kila wiki”

Chelsea ambayo ipo nafasi 3 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu ikicheza jumla ya game 14 na kuwa na point 31, leo itacheza game yake ya 15 ya Ligi Kuu ugenini dhidi ya Wolves, ย Chelsea ikipambania kusogea hadi nafasi ya pili.

Chelsea bado inaendelea kumshawishi Hazard asaini mkataba mpya na wamempa ofa ya mshahara wa pound 300000 kwa wiki ambapo atakuwa ndio mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya club hiyo endapo atasaini ila hataki bado kusaini anasikilizia msimamo wa Real Madrid kwanza.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments