Biko Ad 2
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

DoneDEAL: Man City wamemnasa Riyad Mahrez

on

Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 club ya Man City leo usiku wa July 10 2018 wametangaza rasmi kunasa saini ya staa mpya katika club yao, Man City ambao wanajiandaa na msimu wa 2018/19 ili kutetea taji lao wanazidi kuboresha kikosi chao kwa kufanya usajili.

Man City leo wamefanikiwa kumsajili winga wa kimataifa wa Algeria anayeichezea club ya Leicester City ya England Riyad Mahrez kwa mkataba wa miaka mitano, hiyo ni baada ya kudumu na Leicester kwa misimu minne na kuisaidia kutwaa Ubingwa wake wa kwanza na pekee wa EPL msimu wa 2015/16.

Riyad Mahrez ameondoka Leicester na kujiunga na Man City kwa kiasi cha dau linalotajwa kufikia pound milioni 60, kama utakuwa unakumbuka vizuri Mahrez yupo England toka msimu wa 2014/15 alipojiunga na club ya Leicester City akitokea Le Havre ya Ufaransa.

Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere

Soma na hizi

Tupia Comments