Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Scholes amewakosoa MO Salah na Karius kwa kitendo hiki

on

Jumamosi ya May 26 2018 ulichezwa mchezo wa fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool nchini Ukraine katika mji wa Kyiv na Liverpool kujikutana wakikubali kipigo cha magoli 3-1.

Paul Scholes

Mchezo huo ulimalizika kwa kipa wa Liverpool Loris Karius kukutana na lawama baada ya kuruhusu kufungwa magoli mawili yanayodaiwa kuwa yakizembe, ambayo pia yamechangia kuidhoofisha Liverpool kwa kiasi kikubwa.

Loris Karius

Kiungo wa zamani wa Man United Paul Scholes amewakosoa Loris Karius na Mohamed Salah kwa kitendo chao cha kulia, Karius alilia baada ya kuhisi amewaangisha timu huku Salah alilia wakati akitolewa nje ya uwanja dakika ya 25 kwa kuumia bega baada ya kuvutana na Sergio Ramos.

“Naweza kumuelewa Karius kwa kilichotokea kuwa kinaumiza lakini sio kufikia kulia, kuhusu Salah majeruhi ni sehemu ya mchezo, miaka iliyopita ukiona mchezaji analia ujue ina maana kubwa sana lakini kwa sasa ni tofauti wachezaji wanalialia tu kirahisi”>>>Scholes

Mohamed Salah baada ya kuumia bega

“Binafsi tumeshwahi kupoteza fainali kadhaa najua inaumiza lakini kufikia kulia? hapana sikumbuki kama nimeshawahi kulia katika soka labda nikiwa na umri wa miaka 11 au 12 tukiwa tumepoteza game za fainali”>>>Scholes

Loris Karius

Paul Scholes ni kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya England ambaye amewahi kuichezea Man United kuanzia mwaka 1993 hadi 2011, kwa sasa amekuwa akijihusisha na uchambuzi wa masuala ya soka na amewahi kushinda taji la UEFA Champions League mara mbili akiwa na Man United.

Yametimia maneno ya mchambuzi mkongwe Dr Leaky kuhusu Champions League

Soma na hizi

Tupia Comments