Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

”Wameboresha lakini Huku ni kuwaibia Wanafunzi ”ZAIDI YA MIL 600?’ -TSNP

on

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) leo May 22, 2018 wamezungumza na waandishi wa habari na kutoa malalamiko yao dhidi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/19 uliotolewa na Bodi ya Mikopo mwanzoni mwa mwezi huu wa tano.

Mkurugenzi wa haki za kutetea wanafunzi Gibson Johsonn Eliaform ameipongeza Bodi ya mikopo kwa kuboresha baadhi ya mambo lakini pia ametoa malalamiko kwa kusema  Bodi  hiyo imeendelea kubadilisha vigezo kila mwaka na kuweka vigezo visivyo na tija ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kukwepa majukumu ya kusaidia wanafunzi kutimiza ndoto zao za kupata elimu.

Gibson ameyaeleza baadhi ya malalamiko kuwa ni kipengele no.(vii) kilichotolewa na Bodi ya Mikopo kinachozuia mwanafunzi ambaye mzazi au mlezi wake kama ni mmiliki wa biashara au Meneja wa makampuni yanayotambuliwa na mamlaka kwamba hawataruhusiwa kuomba mkopo, vile vile kipengele kingine ni kile kinachomzuia wanafunzi waliotajwa katika sheria ya utumishi wa umma wasiombe mikopo.

MAGAZETI LIVE: CHADEMA yatoa msimamo kiti cha Mbowe, Sugu Asimamisha Bunge

Soma na hizi

Tupia Comments