Tangaza Hapa Ad

Mix

BREAKING: Rais Magufuli kateua Mkuu mpya wa Majeshi Tanzania anaechukua nafasi ya Mwamunyange

on

Inatokea IKULU Dar es salaam ambapo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya utauzi wa Mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania kama inavyosomeka kwenye hii taarifa hapa chini.

Aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Davis Mwamunyange ni Venance S. Mabeyo ambapo pamoja na kuteuliwakuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Venance anachukua nafasi ya Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu ambapo kitu kingine cha kufahamu ni kwamba Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania, Meja Jenerali James Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance aliyeteuliwa kuwa mkuu wa majeshi.

Uteuzi huu unaanza mara moja ambapo tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadae.

 

ULIPITWA? Tazama hapa chini Makomando wa jeshi la Tanzania wakionyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement