Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Unachotakiwa kujua kuhusu vikao vya bunge vitakavyoanza kesho

on

Ikiwa imesalia siku moja kufika September 6 2016 ambapo mkutano wa nne wa bunge la 11 kuanza, ofisi ya bunge imetoa ratiaba yake kamili ya vikao hivyo ambapo hapa Mkurugenzi wa mawasiliano ya bunge Owen Mwandumbya anaeleza

Mkutano wa nne wa bunge la kumi moja (11) unatarajiwa kuanza kesho Jumanne tarehe 06 Septemba 2016 na kumalizika tarehe 16 Septemba 2016 mjini Dodoma. Shughuli zitakazokuwepo katika mkutano huo ni kama ifuatavyo‘ –Owen Mwandumbya

Katika mkutano huo jumla ya maswali ya kawaida 110 yanatarajiwa kuulizwa na waheshimiwa wabunge na kujibiwa na Serikali. Aidha, maswali 16 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa pia‘ –Owen Mwandumbya

Miswada sita (6) ya sheria ilisomwa mara ya kwanza na kupelekwa kwenye kamati husika ili ifanyiwe kazi. Hivyo katika mkutano wa nne miswada hiyo itashughulikiwa katika hatua zinazofuata (Kusomwa mara ya Pili, Kamati ya Bunge zima na kusomwa mara ya tatu)Owen Mwandumbya

Unaweza kuendelea kumsikiliza kweye hii video hapa chini..

ULIIKOSA HII BAADA YA MAUAJI YA POLISI, TAARIFA HII IKUFIKIE KUTOKA JESHI LA POLISI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement