Tangaza Hapa Ad

Mix

Meya wa Manispaa ya Bukoba ajiuzulu baada ya ripoti ya CAG

on

proxyMadiwani wa Manispaa ya Bukoba wamekua na tuhuma dhidi ya Mstahiki Meya Anatory Amani kwa matumizi mabaya ya madaraka ambapo leo Meya huyo wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani amejiuzulu huku wakuu wa idara tatu wakivuliwa nyadhifa zao akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Khamis Kaputa.

IIIIWakuu waliovuliwa nafasi zao ni pamoja na Mhandisi Nimzihilwa,Ofisa Ugavi Baraka Marwa na Mweka Hazina Ulomi  baada ya kusomwa kwa ripoti hiyo leo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera juu ya kutatua mgogoro uliokuwepo katika manispaa hiyo.

P

OPMiongoni mwa viongozi waliokuwepo ni pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh  na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw.Fabian Massawe.

Picha:Bukobasports.blogspot.com

Tupia Comments

Advertisement