Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kingine alichokisema Soulja Boy kuhusu beef yake na Chris Brown

on

Kumekuwa na majibishano makali kwenye mitandao ya kijamii kati ya rapa Soulja Boy na Chris Brown juu ya kile ambacho kilisemekana kuwa Chris Brown alimpigia Soulja boy simu na kumtishia kumpiga kwasababu tu ali LIKE picha za Karueche ambaye ni mpenzi wa zamani wa Chris.

Muda mfupi baadaye Soulja akaeleza chanzo haswa cha bifu yao ni baada ya Chris kugundua kwamba Rihanna na Soulja Boy walikutana na kuspend time hivyo wivu ukamuingia mpaka akaamua kumpigia simu Soulja.

Imenifikia video ikimuonyesha Soulja Boy akisema kuwa yeye na Chris Brown hawana bifu, na Chris ni kama kaka yake, kama ilivyo kwa watu wengine ndugu hugombana na kupatana hivyo watu wasubirie tu mpambano wa kirafiki kati yake yeye na Chris Brown utakaofanyika March 2017.

#PressPlay #SouljaBoy says #ChrisBrown is his bro and there’s no beef!

A video posted by The Shade Room (@theshaderoom) on

Kwenye mpambano huo bondia Floyd Mayweather atakuwa upande wa Soulja Boy katika kumfunza lakini pia kwa Chris Brown yupo mtu mzima Mike Tyson. Tarehe rasmi za mpambano hazijawekwa ila imetangazwa kuwa March 2017.

Video: Chris Brown Mombasa Rocks Music Festival performance>>>

 

Tupia Comments

Advertisement