Tangaza Hapa Ad

Michezo

Huyu ndio CEO wa Yanga kutoka Ufaransa

on

Ukiachana na headlines za uongozi wa klabu ya Yanga kudaiwa kumleta kocha mpya katika klabu hiyo George Lwandamina kutoka Zesco United ya Zambia taarifa mpya zimetoka Yanga wamemteua mfaransa Jerome Dufourg kuwa afisa mtendaji mkuu wao (CEO).

Yanga wameripotiwa kumpa nafasi hiyo Jerome Dufourg ambaye ni mtaalam wa sports business kufuatia mwenyekiti wao Yusuph Manji kudai kuwa Yanga ilipata hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 1.5 kwa mwaka jana, Dufourg anatajwa kupewa majukumu ya kuendesha shughuli za klabu hiyo na mipango ya fedha.

dcea

Muda wowote kutokea sasa Jerome Dufourg atawasili Tanzania lakini kazi ataanza rasmi November 19 2016, Dufourg amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka la Rwanda pamoja na klabu ya FC Talanta ya Ligi daraja la kwanza Kenya, chanzo cha taarifa hizi ni @shaffihdauda na twitter account ya @JeromeJDufourg

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement