Tangaza Hapa Ad

Mix

Yani nakukumbushia tu kuhusu @NyamaChomaFest 2014 !!!

on

n5

kwa mara ya kwanza kabisa mwaka huu 2014 tamasha kubwa la Nyama choma (The Nyama Choma Festival – TNCF ) limepangwa kufanyika Jumamosi ya March 8.

 

Nani alifikiria kuwa Nyamachoma ingeweza kuwaleta maelfu ya watu pamoja toka lilipoanzishwa? likiwa ni tamasha lililosajiliwa kisheria, limekuwa ni sehemu ya kipekee ya kuenjoy na aina mbalimbali za nyama choma na pia ni eneo linalowakuwakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali wanaofika kufaidi nyama zinazochomwa na wataalamu wa kuchoma nyama kutoka katika kona mbalimbali za jiji la Dar es salaam kwa kuiacha elfu kumi tu geitini.

 

Ukiachana na aina mbalimbali ya nyama zinazokuwepo katika tamasha hili, hii pia ni sehemu mojawapo ya kufurahi na marafiki ikiwa ni pamoja na “mtoko” kwa familia kwani huduma zinazotolewa zimezingatia umri wa watu wote yaani kuanzia watoto hadi watu wazima kukiwa pia na eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya michezo ya watoto, vinywaji vya aina zote na burudani nzuri ya muziki.

Si hivyo tu wapo watu wengine wanaotoa huduma za kahawa, ice cream, michoro ya usoni, vyakula vya kawaida na michezo ya nje ya watu wazima kama pool n.k

 

 

 

n4TNCF wapo katika dunia ambayo inawalazimu kuwa katika mtandao mkubwa na watu wenye weledi tofauti, The Nyama Choma Festival inakuwezesha kuingia katika mtandao huu kwa urahisi zaidi Kwani kwa siku hii moja tu watu wote wanaweka vyeo na nafasi zao kitaaluma pembeni na kuchanganyika na watu

 

Mwaka huu Nyama choma imeamua kuongeza wigo wake zaidi katika sehemu mbalimbali nchini. Ukiachana na Dar es salaam TNCF ilishafanyika Moshi, Arusha na Mwanza na kwa mwaka 2014 itaendelea katika mikoa ifuatayo (Tarehe zinaweza kubadilika)

      Dar es Salaam 08Machi, Arusha 26 Aprili, Mwanza 4Mei,Dar es Salaam 7June, Dodoma 3 Agosti, Morogoro 24 Agosti,Dar es Salaam 6 Septemba,Mwanza 26Oktoba, Dar es Salaam 6 Desemba,Moshi 26Desemba.

n3Toka kuanzishwa kwake TNCF ilipangwa kuwa Tamasha kubwa na maarufu linalofanyika mara nne kwa mwaka likiwakilisha mila ya kitanzania kwa utaalamu wa kuchoma nyama katika miji ambayo inapenda sana nyama choma kikiwa ni chakula maarufu kwa wakazi wa Afrika Mashariki.

Unaambiwa kwa ukarimu wa kitanzania, kila atakayeingia atapewa mshikaki mkubwa na ulionona getini pamoja na kinywaji kisicho na kilevi.

n2

n1

Tupia Comments

Advertisement