DSTV

Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Baada ya jamaa Arusha kutoa siku 30 kwa wezi, ajiandaa kuvunja chungu

on

Tumezoea mtu akituhumiwa kwa wizi anapelekwa mahakamani lakini hii imekuwa tofauti kwenye mila za kabila la Wameru na wamasai Arusha Tanzania, ambapo mtu akikutwa na tuhuma kama za wizi kuna kitu kinaitwa kuvunja chungu. 

Utaratibu wa kuvunja chungu umezoeleka sana kwa makabila yakimeru na kimasai na huvunjwa baada ya makubaliano na huwa kinamhusu ambaye amehusika kama kwa tukio la wizi.

Unaambiwa zamani chungu kilikuwa kikivunjwa, ukoo uliovunjiwa chungu wataanza kufa mashangazi mpaka ukoo unaisha, sasa hivi kikivunjwa analengwa  mhusika au kama wawili walipanga kufanya tukio la wizi.

Sasa Katika kata ya Makuyuni wilaya ya Monduli Arusha Mohamedi Olodi amepanga kuvunja chungu kwa waliomvunjia duka lake na kuiba bidhaa na fedha zenye thamani ya zaidi ya Milioni 2.

MillardAyo.com na ayo TV ilimtafuta ndugu Mohamedi Olodi ambaye amepanga kuvunja chungu hicho na amesema tayari chungu ameshakipata kipo nyumbani kwake na amedai amekuwa akiibiwa dukani mara ya nne sasa na ndani ya wiki hii atakivunja na atakayehusika ni alieona na hajasema, aliyevunja duka pamoja na aliyenunua bidhaa…….

>>>’Basi nikachukua uamuzi wa kuchukua kibali cha chungu na nikapewa siku 30 na zimeshaisha, kuna watu walikuja kuniambia huyo mtu ameshakamatwa nikaenda Monduli nikakatazwa na askari kumuangalia huyo mtu pia kuangalia vitu vyangu wakanimbia nifungue kesi nikashindwa kwa sababu sina kesi kamili, nikachukua hatua ya kuchukua chungu’

>>>’nilikuwa nivunje ile chungu kuna watu waliokuja hapa kuna wakaniambia nisubiri tarehe 12 hivyo kama  mpaka tarehe hiyo hawajatekeleza mimi nafanya mambo yangu’

ULIIKOSA HII YA MTU KUVUNJA CHUNGU ARUSHA? BONYEZA LINK HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement