Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Ciara amethibitisha kuwa na ujauzito wa Russel Wilson

on

Mwanadada mrembo na mwanamziki kutoka marekani, Ciara ambaye baada ya kuachana na rapper Future aliyekuwa baba mtoto wake, na kufunga ndoa na Russel Wilson kupitia mitandao yao ya Instagram yeye na mumewe wameamua kutudokeza  kuhusu ujio wa mtoto wao.

Ciara hakuiweka wazi kama ambavyo mumewe aliandika..yeye alipost na kuandika hivi..

Kwenye siku hii ya birthday yangu nimepokea salamu nyingi za upendo kutoka kwa marafiki na familia…na nina furaha ku share zawadi hii kubwa kuliko zote ambayo mungu amenipatia”

ciara

Kuachana na post hiyo ya Ciara, mumewe Russel Wilson alipost kwenye Instagram yake na kuandika

‘Baraka kubwa kuliko zote. Nashukuru #BabyWilsonOnTheWay”

russsel

Najua kama wewe ni mpenzi wa couple hii utakua umependezwa na habari hii mtu wangu. Kwa Russel Wilson huyu atakuwa mtoto wa kwanza na Ciara atakuwa wa pili.

KAMA ULIMISS ALIKCHOKISEMA MATONYA BAADA YA KUACHIA MDUNDO MPYA, UNAWEZA KUBONYEZA PLAY HAPA MTU WANGU>>>

Tupia Comments

Advertisement