DSTV


Tangaza Hapa Ad

Michezo

FC Barcelona na Iniesta wameingia mkataba wa maisha leo October 6

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania baada ya kuwa katika mazungumzo ya muda mrefu na kiungo na nahodha wao Andres Iniesta hatimae leo October 6 2017 wamefikia makubaliano ya kuingia mkataba mpya wa staa huyo kusalia Nou Camp.

Andres Iniesta awali alikuwa akihusishwa kutokuwa tayari kuongeza mkataba, kitendo ambacho kilimfanya Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu kumshawishi staa huyo, jitihada ambazo zimezaa matunda na kufikia hatua leo hii ya kuingia mkataba wa maisha na staa huyo.

Baada ya Iniesta kuingia mkataba huo alizungumza na kuweka wazo anavyoichukulia siku ya leo “Leo ni siku maalum sana kwangu kwa sababu nabaki nyumbani, nataka kuendelea kufanya vitu muhimu nikiwa hapa”>>> Iniesta

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Iniesta amekulia katika club ya FC Barcelona na ameanza kuitumikia Barcelona B toka 2001 hadi 2002 alipopandishwa timu kubwa, Iniesta hadi sasa akiwa na Barcelona ameshinda jumla ya makombe 30, makombe 8 ya LaLiga, manne UEFA, Copa de Rey 5, Spanish Super Cup 7, UEFA Super Cup 3 na FIFA Club World Cup 3.

VIDEO: Kitu Samatta kaongea kabla ya kucheza na Malawi kesho

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement