PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

AyoTV

“SIELEWI KWA NINI TUMESHINDWA KUWAFUNGA, UCHAWI HAPANA KABISA”-Kocha wa Simba SC

on

Kocha mkuu wa Simba SC raia wa Ubelgiji Patrick Aussems baada ya timu yake kutoka sare tasa dhidi ya watani zao wa jadi Yanga huku wakiwa wameutawala mchezo wao kwa kiasi kikubwa zaidi ya Yanga, Aussems amesema hadi sasa haelewi kwa nini hawajawafunga Yanga.

Simba wamepiga jumla ya mashuti 10 katika lango la Yanga tofauti ya mashuti saba dhidi ya Yanga waliokuwa wamepiga mashuti matatu pekee na kuzidiwa hali ya umiliki wa mpira kwa asilimia 62 kwa 38, hivyo kocha wa Simba Patrick Aussems amekiri kushangazwa na matokeo ya leo.

“Hadi sasa sielewi tumeshindwaje kuwafunga Yanga kutokana na sisi kupata nafasi nyingi, tumeutawala mchezo na kumiliki mpira kwa wakati wote, ninachoweza kusema kwa kila mmoja tulicheza mchezo mzuri na tulistahili kushinda, kuamini ushirikina? mimi Hapana kabisa”>>> Patrick Aussems

Mtoto raia wa New Zealand kaja Taifa kuisapoti Simba ishinde 100-0 vs Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments