Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

UPDATES: Diamond Platnumz, Hamisa warudi tena Mahakamani

on

Leo February 13, 2018 stori inayoshika headlines ni ya Kimahakama ambapo Nyota wa muziki wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao.

Diamond na Mobetto wamefika Mahakamani hapo, ikiwa ni wiki moja baada ya kufika na kusuluhishwa.

Namnukuu Hamisa Mobetto akizungumza nje ya Mahakama  “Maamuzi nimeridhika nayo na tumekubaliana kuhusu matunzo ya mtoto, Pande zote mbili tulikaa na kukubaliana, nashukuru kila mtu tumekubaliana na tumeridhika, hivyo yamekwisha.”

Naye Diamond Platnumz amesema mara ya mwisho ilikuwa ni usuluhishi haikuwa Kesi na leo tumeweka rekodi sawa ili kutunza kumbukumbu na kuweka vitu sawa ili yasije kuzushwa mengine ya uongo na kweli.

“Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani. Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz

Zari saa chache baada ya picha ya Hamisa na videographer wa Diamond

Soma na hizi

Tupia Comments