Top Stories

Maofisa wa Wanyamapori wapandishwa kizimbani kwa kusababishia serikali hasara ya Mil 78

on

Maofisa watatu wa Kitengo cha Matumizi ya Wanyamapori wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 32,599 takriban Tshs Mil 78.

Maofisa hao ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii ni Rajab Hochi, Mohammed Madehele na Isaac Maji wamesomewa makosa yao na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Swai alidai washtakiwa wanakabiliwa na makosa sita mojawapo likiwa ni matumizi mabaya ya madaraka ambalo walilitenda kati ya October 12 na December 31, 2008.

Inadaiwa kosa hilo walilitenda katika Makao Makuu ya Wizara hiyo iliyopo Temeke Dar ea Salaam ambapo wakiwa kama Maofisa wanaowajibika katika kitengo cha Matumizi ya Wanyama pori wakiwa na jukumu la kukusanya mapato yatokanayo na uwindaji walitumia mamlaka yao vibaya kwa kushindwa kukusanya kiasi cha USD 250 kutoka Kampuni ya Uwindaji ya Northern Hunting Enterprises.

Baada ya kusomewa makosa yote sita, washtakiwa walikana, ambapo Wakili Wankyo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo, washtakiwa hao waliepuka kwenda rumande baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na walidhaminiwa wawili waliosaini bondi ya Sh.milioni 50, huku wakitakiwa kutosafiri nje ya Dar es Salaam, ambapo kesi imeahirishwa hadi January 31, 2018.

Walivyofikishwa Mahakamani waliopeperusha Bendera ya Tanzania katika meli

Ilivyokuwa kesi ya Kalugendo ya kuisababishia serikali hasara ya Tsh Bilioni 2.4

Soma na hizi

Tupia Comments