Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Maneno ya Ditto baada ya jina lake kutamkwa kwenye orodha ya Makonda

on

Mwimbaji Ditto ambaye ni mmiliki wa hit single ‘moyo sukuma damu‘ amefafanua kuhusu kilichoendelea baada ya jina la Ditto kusikika kwenye orodha ya Watuhumiwa wa utumiaji/uuzaji dawa za kulevya iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Baada ya jina lake kutajwa baadhi ya watu walianza kumtukana na wengine kumpigia simu nyingi wakidhani ni yeye katajwa lakini ametoa ufafanuzi leo kwamba hakuwa yeye bali ni jina tu lilikosewa na kwamba yuko huru na anaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Amesema amepata usumbufu kiasi chake kwa kupigiwa simu mara kwa mara lakini pia kwa baadhi ya watu kutokujua kwamba jina lilikosewa hivyo wakaanza kumshutumu, kutoa matusi na kumlaumu moja kwa moja.

FULL VIDEO: Paul Makonda akiwataja wanaotuhumiwa kwa biashara na matumizi ya dawa za kulevya, bonyeza play kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement