Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: RC Paul Makonda aelezea alivyosomeshwa na Samuel Sitta

on

Asubuhi ya November 7 2016 watanzania waliamka na habari za kusikitisha baada ya taarifa za kifo cha Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Samwel Sitta ambaye alifariki usiku wa kuamkia November 7 katika hospitali ya Technical University of Munich Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kama ulikuwa hujui Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alisomeshwa na Mzee Samwel Sitta, AyoTV na millardayo.com zimeongea na RC Makonda ambapo amesimulia namna Mzee Samwel Sitta alivyomsaidia….

>>>’Mimi nimesoma kwa kudra za mwenyezi Mungu kwani sikuwa na Mkopo kwahiyo nilikuwa nasoma huku nafanya kazi zangu zilizokuwa zinanisaidia kuendeleza kile nilichokuwa nakisoma shuleni, baadae nikakutana na Mzee Sitta akaniambia natakiwa kurudi shuleni basi ikabidi anilipie ada ya masomo yangu’

>>>’Kwahiyo kuanzia hapo nikamuona yeye zaidi ya Spika wa Bunge bali ni kama mzazi wangu na sikutegemea kama ataweza kunisaidia mpaka nilichukua uamuzi wa kuoa basi yeye aliniambia atasimamia kila kitu kiukweli nilionekana kama mtoto wake wa damu kwa jinsi alivyoonyesha jitihada zake kwangu’-RC Makonda

Bonyeza Play kumsikiliza RC Makonda akizungumza kuhusu kusomeshwa na Samuel Sitta

ULIYAKOSA HAYA YA MTOTO WA MAREHEMU SAMWELI SITTA BASI BONYEZA PLAY HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement