Michezo

EPL: Matokeo ya Man United vs Aston Villa haya hapa

on

IMG_0115.JPG

Ligi kuu ya Uingereza imeendelea jioni ya leo kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja tofauti nchini humo.

Manchester United baada ya kushinda mechi 6 mfululizo katika ligi hiyo, leo walisafiri mpaka Villa Park kwenda kucheza na Aston Villa.

Matokeo ya mchezo huo ni Man United kusimamishwa kasi yao baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na vijana wa Paul Lambert.

Christian Benteke alianza kuifungia goli Villa katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza baada ya kumhadaa beki wa United Jonny Evans na kupiga shuti ambalo De Gea aliliangalia tu likiingia golini.

Kipindi cha pili United walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Radamel Falcao aliyeruka juu na kuunganisha krosi ya Ashley Young.

Pamoja na timu zote kujaribu kupata goli la ushindi lakini mpaka refa anamaliza mechi hiyo ubao wa matokeo ulionyesha Villa 1-1 Man United.

IMG_0116.JPG

Tupia Comments