Tangaza Hapa Ad

Top Stories

AUDIO: Alichokizungumza Moses Machali baada ya kujiunga na CCM kutokea ACT Wazalendo

on

Baada ya kusambaa kwa taarifa ya aliyewahi kuwa Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ikieleza kuwa ameamua kujiunga na chama cha mapinduzi CCM, millardayo.com imempata Moses Machali na amezungumza kuhusu taarifa hiyo.

“Kimsingi ni sahihi hiyo taarifa nimeitoa mimi mwenyewe, kutokana na mwenendo wa Serikali wa awamu ya tano, kwa mtazamo wangu na kwa ufahamu wangu kwa rekodi za nyuma nimekuwa Mbunge ambaye nilikuwa nikipiga kelele sana kuhusu ubadhirifu, kubana matumizi serikalini, nikiwa kama waziri kivuli wa uchukuzi.” – 

“Sasa kwa kumuona Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa wanafanya yale tuliyokuwa tunayataka wapinzani. Mimi nilichoamua ni kuondoka kwenye hivi vyama vya upinzani na kwa uzoefu wangu sioni siasa zinazokua. Nimeamua kung’atuka siku sio nyingi nitachukua kadi” – Moses Machali

Bonyeza Play hapa kupata taarifa kamili.

VIDEO: Maneno ya Afande Sele ambaye ni mwanachama wa ACT Wazalendo kuhusu kujiunga na CCM. Tazama hapa.

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement