Tangaza Hapa Ad

Top Stories

VIDEO: “Mimi sina ugomvi na Profesa Lipumba” – Katibu Mkuu CUF

on

Kiongozi wa C.U.F Maalim Seif amekaa mbele ya Wanahabari November 27 2016 Dar es salaam na kuongelea mambo mbalimbali, miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni kama yeye na aliyekua Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Lipumba wana ugomvi?

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad amesema kuwa yeye hana ugomvi wowote na anayetajwa kwasasa kuwa ndiye mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibahim Haruna Lipumba kama inavyodaiwa au kusemwa na wanachama walioko upande wake, isipokuwa tofauti ipo kati ya Lipumba, kundi lake na Chama.

“Mimi sina ugomvi na Lipumba hata kidogo, Lipumba ana ugomvi na chama na kundi lake maamuzi yamechukuliwa na mkutano mkuu wa taifa hata ukinikutanisha mimi na Lipumba siwezi kubatilisha maamuzi ya mkutano mkuu wa chama ambayo yaliwafukuza uanachama chini ya baraza kuu la uongozi” – Maalim Seif Hamad

VIDEO: Katibu Mkuu wa CUF Seif Sheriff Hamad amezitaja sababu zilizofanya azuiliwe kufanya mkutano Mtwara pamoja na kupewa kibali cha Polisi

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement