Duniani

Watanzania wawili kwenye Tamasha la Filamu Ufaransa

on

Cannes Film Festival ni tamasha kubwa Filamu Duniani ambalo hufanyika kila mwaka ambapo mwaka 2017 limefanyika mara ya 70 tangu kuanzishwa kwake September 20, 1946.

Tamasha hilo huhudhuriwa na watu maalumu kutoka sehemu mbalimbali duniani ambapo mwaka 2017 Watanzania Ernest Napoleon na Miriam Odemba wakiwa miongoni mwa waliobahatika kupata nafasi ya kuhudhuria.

Wakati Ernest akialikwa kama Raisi wa Kampuni ya utengenezaji na utayarishaji  wa Filamu Marekani D Streets MediaMiriam Odemba amealikwa kuwakilisha Kampuni ya Chopard ambayo inaongoza kwenye utengezeaji wa vito vya thamani.

Picha za Ernest na Miriam Odemba zilisambaa weekend wakiwa kwenye Red Carpetkwenye mji mdogo wa Cannes, Ufaransa kwenye tamasha ambalo Filamu mbalimbali hufanyiwa review na Filamu moja hupewa tuzo na mara nyingi filamu zinayopata tuzo kwenye Cannes Film Festival hupata tuzo za Oscars Marekani.

Ernest Napoleone na Miriam Odemba katika pozi la Red Carpet kwenye Tamasha la Filamu Ufaransa

 

Soma na hizi

Tupia Comments