Tangaza Hapa Ad

Burudani

U-HEARD: Alichosema Fid Q baada ya picha za Ben Pol kuwa gumzo

on

Kati ya story ambazo zina-make headlines kwa sasa ni pamoja na picha za Mwimbaji wa R&B kutoka Bongoflevani Ben Pol alizoziweka kwenye account yake ya Instagram ambazo zimekuwa gumzo.

Picha hizo zinamuonesha staa huyo akiwa mtupu na amefungwa kamba ambapo kutokana na kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii na kupitia U-heard ya XXL ya Clouds FM Mtangazaji Soudy Brown alipiga story na Fid Q pamoja na Ben Pol ili kujua undani kuhusu picha hizo.

“Hiyo Idea mimi sihusiki nayo, sijui alikuwa anataka kuongelea nini kwenye ile cover japo wazo limekaa kama anatafuta kiki lakini binafsi sijioni huko, siwezi kuhukumu.” – Fid Q.

Ben Pol alipopigiwa simu na Soudy Brown ilionekana kama hakuwa sehemu nzuri hivyo akamwambia Soudy >>> “Soudy ngoja nitoke hapa nilipo halafu ntakupigia tena.”

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story…

ULIPITWA? Tazama hapa chini Wabongo walivyovaa kizamani kwenye party ya Sallam

EXCLUSIVE: Aliyesali kwa sauti gari lisisombwe na maji afunguka, play hapa chini kumtazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement