Biko Ad
CRDB Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Kilichojiri leo kesi ya Ofisa wa TRA anayemiliki magari 19

on

Upande wa mashtaka unatarajia kumsomea maelezo ya awali (Ph), Ofisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa na kosa la kukutwa akimiliki magari 19, mali isiyolingana na kipato chake, January 11, 2018.

Mushi alitarajiwa kusomewa (Ph) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambapo aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi January 11,2018 ambapo mshtakiwa huyo atasomewa maelezo hayo ya awali (Ph).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mushi anadaiwa kuwa kati ya March 21,2016 na June 30, 2016  jijini Dar es Salaam  akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimiliki magari 19.

Ulipitwa na hii? MAHAKAMANI: Kesi ya Aveva na Malinzi

 

Soma na hizi

Tupia Comments