Top Stories

Wapenzi wavalishana pete ya uchumba na kuoana ndani ya saa 2 na hii ndio sababu (Pichaz+)

on

Tukiweka pembeni stori  inayovuma sana tokea Marekani ya kitabu cha Fire and Fury leo January 9, 2018 nimeipata nyingine ya  wapenzi wawili  Nicole na Danny Rios wanaoishi New York nchini Marekani siku za hivi karibuni wamefunga ndoa ndani ya masaa mawili tu baada ya kuvalishana pete ya uchumba.

Hii ilitokea baada ya mwanaume kufanya maandalizi ya matukio yote mawili kwasababu mpenzi wake Nicole anaumwa ugonjwa wa Lupus ambao si ugonjwa wa kupona.

Lupus ni ugonjwa ambao hutokea pale ambapo mfumo wa kinga mwilini mwa binadamu unazishambulia tishu za afya ya mwili badala ya kushambulia vijidudu vinavyoleta madhara mwilini kama ambavyo imezoeleka. Ugonjwa huu huwa na madhara zaidi kama mgonjwa husika atakuwa na stress za aina yoyote.

Danny ameieleza BBC kuwa alifanya hivyo kuepusha mpenzi wake huyo Nicole kupata stress za kuandaa harusi kwa kushiriki kwenye maandalizi yote baada ya kuvalishwa pete ya uchumba, na hivyo Danny akaona kufanya matukio yote mawili kwa wakati mmoja kutaepusha stress hizo.

Wawili hao walikuwa wamesafiri kwenda Walt Disney World nchini Marekani ili kusherehekea birthday ya Nicole na walivyorudi nyumbani wakakuta kila kitu kiko tayari.

“Tulivyorudi tulikuta wamepamba vizuri na nikahisi wazazi wake wamepamba kwa ajili ya Krismasi lakini tulivyoingia ndani nikakuta watu wengi, ndugu, jamaa na marafiki na ndipo Danny aliponivalisha pete,”– Nicole

“Baada ya hapo alinipeleka ndani na kueleza sababu ya kufanya hivi na kuomba tufunge ndoa muda huo huo kama nitaridhia kwani kila kitu kilikuwa kimeandaliwa tayari kwa harusi.” – Nicole

Soma na hizi

Tupia Comments