Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Ilivyokuwa Mahakamani katika kesi Lema na watuhumiwa 61 wa ugaidi

on

Kutoka jijini Arusha kwenye habari zilizojiri Mahakamani leo February 13, 2018 ni pamoja na kesi ya watuhumiwa 61 wa ugaidi jijini humo ambayo imeshindwa kuendelea kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kuwa haujakamilika.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Christina Kisinda ameahirisha kesi hiyo hadi February 27 mwaka huu ambapo itakuja kwa ajili ya kutajwa tena.

January 16, 2018 watuhumiwa hawa walivua nguo Mahakamani kwa madai ya upelelezi kuchukua muda mrefu bila kukamilika, hata hivyo January 30 mwaka huu zaidi ya watuhumiwa 20 walihukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kugoma kuingia Mahakamani kwa ajili ya kesi yao.

Wakati huo huo Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema amewasilisha hoja za kukata rufaa katika Mahakama Kuu akidai Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yake ameshindwa kusimamia mwenendo wa kesi hiyo na kupinga kitendo cha Hakimu huyo kuendelea kusikiliza kesi hiyo ikiwa wamekwishakata rufaa ya kutotaka kuendelea naye.

kesi hiyo imeahirishwa hadi June 15 mwaka huu.

“Nawatakia kazi njema, kafanyeni kazi” -Rais Magufuli

GOOD NEWS: Reli ya kati imefunguliwa, TRL imepoteza Bilioni 4

 
 

Soma na hizi

Tupia Comments