Tangaza Hapa Ad

Michezo

KRC Genk ya Samatta imeshindwa kuvunja rekodi ya historia Ubelgiji

on

Usiku wa April 20 2017 michuano ya robo fainali ya UEFA Europa League iliendelea tena kwa michezo ya marudiano ya robo fainali kuchezwa, timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wake wa nyumbani wa Luminus Arena.

Mchezo huo kati ya KRC Genk dhidi ya Celta Vigo ilikuwa ni mchezo ambao KRC Genk walikuwa na mtihani wa kuvunja rekodi nzito ya Celta Vigo ambapo katika historia hawajawahi kufungwa na timu za Ubelgiji katika mashindano ya UEFA Europa League licha ya kuwa msimu huu ndio mara ya kwanza kwa Genk na Celta Vigo kukutana.

Genk wameondolewa na Celta Vigo katika hatua hiyo kwa jumla ya magoli 4-3, hiyo ni baada ya leo kutoka sare ya 1-1 kwa goli lililofungwa na Trossard dakika 67 baada ya Sisto kuifungia Celta Vigo goli la uongozi dakika ya 63 lakini Genk walifungwa kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kwanza uliyochezwa Balaidos.

VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement