Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Binadamu aliyegeuka fisi baada ya kukosewa masharti ya mazishi…

on

October 5, 2016 kupitia Leo Tena ya Clouds FM, Mtangazaji Geah Habib amekutana na stori huko Mtwara juu ya mwanaume mmoja aliyekua mganga wa kienyeji, mtu huyo inadaiwa kuwa alitoa masharti kwa watoto wake kwamba siku akija kufa basi mwili wake usitolewe kupitia mlangoni badala yake wavunje ukuta na kisha azikwe na nguo nyeusi.

Inasemekana kwamba baada ya kufariki watoto wake hawakutekeleza suala hilo na ndio jambo linatajwa kuwa limesababisha akageuka kuwa fisi ambaye anasumbua watu na kula mifugo kila wakati.

>>>>Kwa taarifa zilizopo kuhusu anakotokea huyo fisi wanadai alikuwa mganga wa kienyeji na alitoa masharti akisema siku nikifa mnizike bila sanda mnivishe nguo nyeusi, mbomoe ukuta ndo mtoe maiti msinitolee mlangoni sasa inadaiwa kuwa wale ndugu zake hawakufanya alivyotaka ndio ikatokea, nafikiri kuna mambo ya kiimani kwamba alitoka akaenda maeneo ya likondwe, mkunwa mpaka maeneo ya dihimba huko amefanya vurugu zake ndio karudi huku kwetu:- Shuhuda

Sikiliza full stori kwa kubonyeza Play hapa.

ULIMISS KAULI YA BABA YAKE NGASSA KUHUSU USHIRIKINA KWENYE SOKA? TAZAMA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement